JE WEWE UKIKATWA MASIKIO YATAOTA MENGINE KAMA YA HUYU?

Nadhani unamfahamu konokono.Konokono wako wa aina mbalimbali,kuna wale ambao wanaishi na nyumba zao na kuna ambao wanaishi bila kuwa na nyumba zao.Mara nyingi nyumba za konokono
hutumika kama mapambo ya ndani baada ya konokono kufa.

Nyumba hizo za konokono ambazo ni mapambo hupatikana kwa wingi maeneo ya ufukweni mwa bahari na mitoni ama mazingira yenye majimaji.

Hayo ni tisa,kumi konokono ana vitu vinavyoitwa papasio. Papasio hizo konokono huzitumia kama macho na pia kama dira kupata mwelekeo wakati anapotaka kutoka eneo moja kwenda jingine.
Pia papasio hizo huzitumia kuhisi vitu mbalimbali vya hatari au vizuri kwake. 

Cha kustaajabisha ukizikata papasio zote mbili za konokono,baada ya muda zitaota zingine na kuwa kama zilivyokuwa awali.
   
Je wewe ukikatwa masikio yataota mengine?

Post a Comment