Boko haramu waua tena nchini Nigeria



Wanamgambo wa kundi la Boko Haram huko kaskazini mwa Nigeria wamevamia kituo cha polisi, banki na mahakama na kuwaua maafisa saba wa polisi na raia.
Duru zinaarifu kuwa hujuma hiyo ilijiri Jumatano katika mji wa Gwaram katika jimbo la Jigawa ambapo vikosi vya usalama vilikabiliana na wanamgambo hao kwa muda wa masaa kadhaa. Jimbo la Jigawa linapakana na jimbo la Yobe ambalo ni ngome ya Boko Haram. Jimbo hilo ni kati ya majimbo matatu ya kaskazini mashariki mwa Nigeria ambayo yako katika hali ya hatari.
Maelfu ya watu wamepoteza maisha nchini Nigeria tokea kundi la Boko Haram lianzishe uasi mwaka 2009. Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha nchini hitilafu za kidini na kikabila.

1 comments:

Post a Comment