Home »
Unlabelled »
Wapinzani Kenya wakosoa operesheni ya usalama
Nchini Kenya viongozi wa muungano wa Cord, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wamekosoa jinsi serikali inavyoendesha msako unaolenga kuwanasa washukiwa wa ugaidi nchini.Wakizungumza katika maeneo tofauti, viongozi hao walisema kuwa msako huo, unawaathiri hata raia wasiokuwa na hatia. Akizungumza na gazeti la kila siku la Taifa Leo akiwa Marekani, Odinga amesema kuwa amesikitishwa na jinsi serikali inavyoendesha operesheni ya kukabiliana na makundi ya kigaidi hususani katika mtaa wa Eastleigh, jijini Nairobi. Odinga amesema kuwa si jamii ya Wasomali pekee ndiyo inayohusishwa na vitendo vya ugaidi nchini Kenya, kwani washukiwa wa ugaidi kutoka katika jamii mbalimbali kama vile Waluo, Waluhya, Wakikuyu na jamii nyinginezo wamewahi kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya ugaidi. Wakati huohuo, Musyoka amekosoa amri iliyotolewa hivi majuzi ya kuwapiga risasi washukiwa wa uhalifu na kusema kuwa inakiuka katiba. Makamu huyo wa zamani wa rais wa Kenya, amesema kuwa yeye akiwa mwanasheria, hawezi kuunga mkono amri hiyo ya kuua na kuongeza kuwa mshukiwa hana hatia hadi mahakama ithibitishe vinginevyo. Amesema kuwa tatizo la ukosefu wa usalama ambalo limeikumba nchi limesababishwa na maafisa wafisadi ambao wanalinda vizuizi vilivyoko barabarani. Hata hivyo, serikali ya Kenya Jumanne ilikanusha madai kuwa inalenga jamii ya Wasomali katika operesheni ya usalama inayoendelea nchini hum
Post a Comment