Musharaf anusurika kifo....




Polisi imetangaza kuwa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Parviz Musharaf ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini, amenusurika jaribio la kutaka kumuua baada ya bomu kulipuka muda mfupi kwenye eneo msafara wake ulipokuwa ukipita.
Ripoti zinasema kuwa, bomu hilo lilitegwa kwenye eneo lililopangwa kupita msafara wa Musharraf alipokuwa akitoka hospitali ya jeshi alikokuwa amelazwa kutokana na matatizo ya moyo. Hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenye mlipuko huo na wale kundi lililotangaza kuhusika.
Musharraf aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan mwaka 1999 hadi 2008 alirejea nchini humo Machi mwaka jana ili kugombea uchaguzi mkuu lakini alizuiwa kufanya hivyo na kukabiliwa na mashtaka kadhaa ukiwemo uhaini.

Post a Comment