ASKARI WA MAREKANI AFANYA MAAFA....



Askari wa Marekani katika kambi ya jeshi ya Fort Hood kwenye jimbo la Texas amewaua watu wanne kwa kuwapiga risasi na kujeruhi wengine 14.
Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa, askari huyo aliyewamiminia watu risasi Ivan Lopes aliyekuwa na umri wa miaka 34 alijipiga risasi baada ya mauaji hayo na kwamba amefariki dunia kutokana na majereha. Mwaka 2009 pia kambi hiyo ya jeshi ya Marekani ilishuhudia vitendo vya kufyatuliana risasi ambapo watu 13 waliuawa na wengine 30 kujeruhiwa. Katika tukio jingine la kupigana risasi lililojiri mwezi Septemba mwaka uliopita katika kambi ya Jeshi la Anga la Marekani mjini Wasington, askari mmoja aliwaua watu 12 kabla na yeye kupigwa risasi na polisi na kuuawa.
Fort Hood ni miongoni mwa kambi za kijeshi za Marekani zenye idadi kubwa ya askari, ambayo ilituma askari wengi zaidi katika vita vya Iraq kuliko kambi nyingine za kijeshi za nchi hiyo.

Post a Comment