MITANDAO MINGI ZAIDI YA KIJAMII YAMEENDELEA KUUNGA MKONO NDOA YA JINSIA MOJA...
in
KIMATAIFA
- on 3:46 PM
- No comments
Siku chache zilizopita tulisoma habari ya kujiuzulu Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya kutengeneza Programu za Kompyuta ya Mozila yenye makao yake nchini Marekani. Brendan Eich alilazimika kuachia
ngazi kutokana na mchango wake wa kifedha kwa makundi yanayopinga ndoa za watu wa jinsia moja. Mwaka 2008 Brendan Eich alitoa mchango wa dola 1000 kwa kundi lililokuwa likipinga kuidhinishwa uchafu huo katika jimbo la California nchini Marekani. Hatua ya bodi ya wasimamizi wa Mozila ya kumshinikiza Eich ajiuzulu kutokana na misimamo yake ya kupinga ndoa za watu wa jinsia moja inaashiria jinsi shirika hilo linavyoweza kwenda katika kutetea uozo huo. Uchunguzi wa kina unafichua jinsi mashirika mengine makubwa ya Marekani yanavyotoa misaada ya hali na mali kutetea na kuunga mkono vitendo vichafu vya liwati na usagaji. Gazeti la Ufaransa la Libération limeandika kuwa, makampuni mengine ya Marekani kama vile Apple, Google na Facebook yamekuwa katika msitari wa mbele kupigia chapuo ndoa za watu wa jinsia moja. Wafanyakazi wa mashirika hayo ambao hawakubaliani na uchafu huo hutishwa na wakati mwingine hulazimishwa kujiondoa. Mwaka wa 2008, shirika la Apple ambalo linatengeneza simu mashuhuri za mkononi za Iphone na vifaa vingine kama vile Ipad ilitenga kiasi cha dola laki moja kwa ajili ya kuunga mkono liwati na usagaji katika kalibu ya kile kinachodaiwa kuwa ni haki za binadamu. Shirika hilo limekwenda mbali zaidi na kwa sasa limewataka wajumbe wa bunge la Kongress kupitisha sheria itakayosahilisha kuajiriwa mashoga na wasagaji kwenye mashirika makubwa ya nchi hiyo.
Kwa masikitiko makubwa, hujuma hiyo dhidi ya taasisi za ndoa na familia nchini Marekani inaendeshwa pia na watu wenye nguvu na ushawishi wa kifedha na kisiasa. Hivi majuzi, jaji wa mahakama moja nchini humo Orlando Garcia alitangaza waziwazi kuwa anaunga mkono ndoa za mashoga na wasagaji katika jimbo la Texas ambapo alisema "Katika jamii 'iliyo huru' watu wanapaswa kujiamulia wayatakayo hata kama ni kuoana mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke"
Kwa mtazamo wa haraka ni kwamba, serikali kuu ya Marekani inachukulia ndoa za watu wa jinsia moja kuwa sawa na ndoa za kawaida ambazo ni kati ya mwanaume na mwanamke na kwa mantiki hiyo kumekuwa na harakati nyingi za kisiasa za kutaka mashoga na wasagaji pia wapate haki sawa na watu waliofunga ndoa za kawaida. Harakati hizo zimeonekana kushadidi na kushika kasi katika kipindi cha uongozi wa Rais Barack Obama. Kiongozi huyo ametajwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani kutangaza hadharani na kuonyesha kivitendo uungaji mkono wake kwa mashoga na wasagaji nchini humo na duniani kote. Inafaa kukumbusha hapa kuwa, ndoa za watu wa jinsia moja zimehalalishwa na kuruhusiwa kisheria katika baadhi ya majimbo ya Marekani ingawa majimbo mengine yamepiga marufuku ndoa za aina hiyo. Takriban majimbo 20 kati ya majimbo yote 50 ya Marekani yameidhinisha liwati na usagaji. Mwaka 2004, jimbo la Massachusetts lilikuwa la kwanza kuidhinisha na kutambua kisheria ndoa za watu wa jinsia moja. Wanaopigia chapuo uchafu huo nchini Marekani wamehakikisha kwamba hata katika jeshi suala hilo linaidhinishwa na mashoga na wasagaji wanaruhusiwa kuhudumu kwenye jeshi la taifa.
Wachambuzi wengi wanasema bahari ya maadili bora Marekani inazidi kuchafuliwa na meli zilizosheheni ufuska na uozo wa kila nui. Inaaminika kwamba, Wamarekani wanaotetea maadili bora na kupinga hujuma dhidi ya taasisi za ndoa na familia, kwa sasa wanakabiliwa na hatari kubwa kuliko wakati wowote ule katika historia ya nchi hiyo.
Post a Comment