WANANCHI WAFURAHIA UCHAGUZI...
















 BBC.
Raia nchini Afghanistan wanasherehekea kile kinachoonekana kama uchaguzi wa urais wa amani licha ya vitisho vya ghasia vilivyotolewa na kundi la Taleban

Wengi walicheza densi katika barabara za mji mkuu wa Kabul huku wengine wakionyesha vidole vyao vilivyopakwa wino, kama ishara ya kukaidi agizo la Taleban la kutoshiriki katika shughuli hiyo muhimu.
Baadhi ya raia hatahivyo walishindwa kupiga kura kutokana na ukosefu wa makaratasi ya kupigia kura yaliosababishwa na idadi kuu ya watu waliojitokeza.
Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa kufikia sasa imepata malalamishi 160 kuhusu udanganyifu katika shughuli hiyo.
Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea lakini matokeo rasmi hayatarajiwi kutolewa hivi karibuni



Post a Comment