Waziri Mkuu wa Mali Oumar Tatam Ly na serikali yake wamejiuzulu ikiwa ni miezi sita tu tangu ashike wadhifa huo.
Hata hivyo haijaelezwa ni kwa nini waziri mkuu huyo ameamua kuacha kazi. Taarifa iliyotolewa na Rais Ibrahim Boubacar Keita imeeleza kuwa, Oumar Tatam amewasilisha barua ya kujiuzulu serikali nzima kwa rais huyo na kwa ajili hiyo Moussa Mara aliyekuwa waziri wa mipango ya miji ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Mali.
Waziri Mkuu huyo mpya ambaye ni mwanasiasa maarufu aliyegombea pia katika uchaguzi wa rais mwezi Agosti uliopita, atabeba jukumu la kuwatea mawaziri wapya ingawa bado muda haujainishwa wa kufanya hivyo. Keita alichaguliwa katika uchaguzi wa kwanza wa rais uliofanyika nchini Mali tangu mwaka 2007, ikiwa ni baada ya nchi hiyo kutumbukia katika mgogoro wa ndani mwanzoni mwa 2012 baada ya waasi wa Tuereg kufanya uasi uliofuatiwa na mapinduzi ya kijeshi.
Post a Comment